3 Mei 2025 - 17:02
Hujjat-ul-Islam Aali: Msaada kwa wengine unarudishwa (unafidiwa) mara nyingi zaidi na Mwenyezi Mungu

Mwalimu wa chuo kikuu na shule ya kidini alieleza kuwa kusaidia na kutatua matatizo ya wengine ni chanzo cha kupata malipo mengi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Alisisitiza kwamba sehemu ya kila mtu katika neema ya Mwenyezi Mungu inategemea uwezo wake wa kupokea, na ili kufaidika zaidi, ni lazima kuongeza uwezo huu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) – ABNA – Hujjat-ul-Islam Masoud Aali, Ijumaa usiku, tarehe 2 Mei, 2025, katika hafla ya Sherehe ya 'Siku Kumi za Karama', iliyofanyika katika Mji wa Astaneh-ye Ashrafiyeh, alizungumzia umuhimu wa heshima ya ki_Mungu katika ukuaji wa kiroho wa binadamu na kusema: "Rehema, heshima na ukamilifu wa Mwenyezi Mungu ni katika mambo yasiyokuwa na mwisho, na kama Wanadamu wangeweza kuwa na uwezo kama wa Mitume (na Manabii amani iwe juu yao), Mwenyezi Mungu angeliwapa kulingana na uwezo wao."

Mtaalamu huyu wa kidini aliongeza: "Neema isiyo na mwisho ya Mwenyezi Mungu ipo, na sehemu ya kila mtu katika neema hii inategemea uwezo wake wa kupokea. Hivyo, kama mtu amekosa, hiyo ni kwa sababu ya udhaifu wa uwezo wake, na ni lazima apanue uwezo wake."

Akizungumzia kuhusu jukumu la Ahlul-Bayt (a.s) katika malezi ya kiroho ya wanadamu, alisema: "Katika mafundisho ya Qur’an na tabia za Ahlul-Bayt (a.s), kukua kwa uwezo wa kiroho wa binadamu ni jambo la umuhimu mkubwa, kwa sababu kadri mtu anavyotoka katika ubinafsi, ndivyo atakavyokuwa na sehemu kubwa zaidi ya ukamilifu."

Hujjat-ul-Islam Masoud Aali alisisitiza umuhimu wa kuwa na mtazamo mpana wa jamii na alisema: "Katika mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s), kuona mahitaji ya wengine na kuwa na mtazamo wa kina kuhusu jamii ni dalili ya ukubwa wa mtu."

Aliendelea kusema: "Panua mtazamo wako, kwa sababu kuongoza nyoyo ni muhimu, na ili kufikia ukuu, ni lazima upanue uwezo wako."

Mwalimu huyu wa chuo kikuu na shule ya kidini alielezea kumsaidia mtu mwingine na kutatua matatizo yake kama moja ya kanuni muhimu za kimaadili katika mafundisho ya Kiislamu na kusema: "Ikiwa utakuwa njia ya wema kwa wengine, Mwenyezi Mungu atakurudishia (atakufidia) mara nyingi zaidi."

Akizungumzia umuhimu wa kutambua upande wa haki na kusaidia upande huo, alisema: "Wote wanaoishi katika mstari wa haki, katika historia na katika ulimwengu, wanahesabiwa kama sehemu ya upande wa haki, na wale waliopo nje ya mstari huo ni sehemu ya upande wa batili."

Hujjat-ul-Islam Masoud Aali alimaliza kwa kusema: "Ikiwa utamkumbuka Imam Hussein (a.s) na kutamani kuwa katika upande wa haki, basi wewe ni kama wale walio katika vita sambamba na Abi Abdillah (a.s) na wakapata Shahada."

Alizungumzia pia mchango wa Shahidi Haji Qasem Soleimani katika upande wa haki na kusema: "Shahidi Soleimani ni mfano wa jamii iliyojiandaa kutoa maisha yao katika njia ya haki. Hivyo, ni muhimu kuona kwa umakini pande zote mbili na kujua kuwa kila mahali ambapo maadui wa Uislamu wanajaribu kumdhuru Kiongozi, Jeshi, Hizbollah, na viongozi wa dini walio wema (Marajii), kufanya hilo ni kuwa sehemu ya upande wa haki."

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha